Jumatatu , 10th Jul , 2023

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, amewataka wataalamu wa afya nchini  kupunguza semina ili kuwa na muda zaidi wa kutoa huduma bora za matibabu kwa wananchi. 

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu,

Waziri Ummy ameyasema hayo leo Julai 10, 2023 katika ziara yake mkoani Simiyu wakati akizungumza na viongozi wa mkoa huo chini ya  Mkuu wa Mkoa Dkt. Yahaya Nawanda.

"Wataalamu wa afya punguzeni semina maana mmekuwa na semina nyingi hadi kupelekea wagonjwa kukosa huduma kwa wakati na kumekuwa na msomgamano mkubwa katika vituo vya kutolea huduma za afya sababu ya semina," amesema Waziri Ummy

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa katika utolewaji wa huduma za afya nchini hakuna kilichosimama kwakuwa serikali imejenga majengo ya hospitali, imetoa dawa na vifaa tiba, hivyo ni jukumu la wataalamu wa Afya kutoa huduma bora patika vituo hivyo. 

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Simiyu Dkt. Yahaya Nawanda amemhakikishia Waziri Ummy kuwa Mkoa huo utaendelea kupunguza vifo vya mama na mtoto ambapo hadi sasa kuna vifo 29 toka mwaka 2022.