Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron akiongea nje ya Downing Street
Katika taarifa yake aliyoitoa nje ya Ofisi za Downing Street, Cameron amesema atajaribu kuliongoza jahazi la taifa la Uingereza kwa wiki chache zijazo na miezi, lakini kiongozi mpya anahitaji sasa.
Waziri Mkuu Cameron alikuwa akiwasihi wananchi kutojitoa Umoja wa Ulaya, alishindwa kwa kura asilimia 52 dhidi asilimia 48 licha ya London, Scotland na Ireland ya Kaskazini kunga mkono kubakia EU.


