Waziri Bashungwa akizungumza Makao Makuu ya JKT Chamwino mkoani Dodoma amesema mitambo hiyo ya kilimo itawezesha jeshi hilo kuwa na mipango mizuri ya uzalishaji chakula
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Stergomena Tax ambaye aliasisi ununuzi wa zana hizo akiwa Waziri wa Ulinzi amesema zana hizo zitasaidia kukabili upungufu wa utekelezaji wa mradi wa umwagiliaji wa mashamba ya kimkakati ya Chita na Mngeta.