Naibu Waziri wa Maji, Juma Aweso
Mhe. Aweso amesema hayo mara baada ya kupokea taarifa ya hali ya upatikanaji wa maji mkoani Geita akiwa katika ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maji wilayani Chato.
"Mhe Mkuu wa Mkoa mim naomba niwaombe radhi wana Nyang'wale kwa hiki kilichotokea, lazima tubanane sisi wenyewe kuhakikisha maji yanapatikana na lazima maji yafike Nyang'wale", Amesema Naibu Waziri Aweso.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA, Mhandisi Nicas Ligomba ameelezea sababu zilizosababisha mradi huo kusuasua kwa miaka mingi kuwa ni kutokana na uwezo mdogo wa mitaji.
Mara baada ya kupokea taarifa hiyo, Naibu Waziri Aweso alifika wilayani Chato na kukagua mradi mkubwa wa maji wa Inchwakima Imalabupina ambao kwa sasa unahudumia wakazi wapatao 14,131.