Ijumaa , 9th Mei , 2014

Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii nchini Tanzania Dk. Self Rashid amekitaka chama cha msalaba mwekundu kuwatumia vijana mashuleni kwa kuwapatia mafunzo ya utoaji huduma za kibinadamu ili huduma zitolewazo na chama hicho ziwe endelevu.

Dk. Self Rashid ametoa wito huo kupitia katika hotuba yake iliyosomwa na mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro kwenye maadhimisho ya siku ya chama cha msalaba mwekundu duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Mbeya

Kwa upande wake makamu wa Rais wa chama cha msalaba mwekundu nchini Tanzania Dk. Zainab Gama amesema chama cha msalaba mwekundu kimekuwa kikifanya kazi zake bila upendeleo kwa kutoa misaada ya
kibinadamu wakati wa majanga, huku akiitaka serikali kupitia wizara ya sheria na katiba kutunga muswada wa marekebisho ya sheria ili upitishwe na bunge na hatimaye kuwa sheria itakayosaidia chama chicho kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi.