Jumamosi , 4th Dec , 2021

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Mwigulu Nchemba amesema katika Taifa la Tanzania uhalisia ni kwamba kati ya vijana 100 wanaoingia kwenye soko la ajira, ni vijana saba tu ndio wanaopata ajira kwenye sekta rasmi.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Mwigulu Nchemba.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa mahafali ya 35 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kampasi kuu ya Dodoma, ambapo amewataka wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuwa tayari kuwasaidia vijana wanaohitimu elimu ya juu ili waweze kuingia kwenye soko la kujiajiri kwa kujiamini wakati serikali ikiendelea na jitihada za kukuza ajira rasmi.

Katika hatua nyingine amewaagiza watendaji na watalaamu wa chuo hicho kupanua wigo wa huduma za utafiti ambazo ni muhimu katika kutatua changamoto mbalimbali za kimaendeleo zinazowakabili wananchi.