
Maelfu ya wazee kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania leo wamefanya maandamano ya amani katika mkoa wa Ruvuma, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kilele cha Siku ya Wazee Duniani na Kitaifa, ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 1 Oktoba.
Maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kauli mbiu isemayo: "Wazee Tushiriki Uchaguzi Mkuu kwa Ustawi wa Jamii Yetu" kauli mbiu ambayo inalenga kuhamasisha ushiriki wa wazee katika mchakato wa kidemokrasia, hususan katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu ujao Oktoba 29 mwaka huu.