Mkuu wa Wilaya ya Arusha Christopher Kangoye akizungumza katika uzinduzi wa juma la chanjo.
Kumekuwepo na mpango hapa nchini unaohamasisha wazazi wote kushirikiana kwa pamoja, na kuwabeba jukumu la kuwapeleka watoto wao katika vituo vya afya ili kupata taarifa za maendeleo ya watoto wao kwa pamoja hamasa inayoonekana kushindwa kupata matokeo mazuri katika baadhi ya maeneo nchini.
Wakati Tanzania ikikabiliwa na ongezeko la vifo vya watoto zaidi ya milioni mbili kwa mwaka wenye umri wa chini ya miaka mitano vinavyotokana na magonjwa mbalimbali ikiwamo yale ya kuambukizwa, wito umeendelea kutolewa ambapo safari hii Mkuu wa Wilaya ya Arusha Christopher Kangoye akizungumza katika uzinduzi wa juma la chanjo amesema mwitikio wa akinababa hauridhishi.
Mwito kwa wanaume kushiriki kikamilifu katika masuala ya huduma ya mama wajawazito pamoja na Afya ya mtoto, umetiliwa mkazo na Mwenyeki wa kamati ya huduma ya Afya katika Jiji la Arusha Isaya Doita,
Kwa upande wake mganga mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Arusha Jane Barakwililiza akibainisha lengo la chanjo inayotolewa sasa kuwa ni juhudi za serikali kuhakikisha inatimiza wajibu wa kuondoa vifo vinavyozuilika kupitia chanjo.
Ushiriki wa wazazi katika zoezi la chanjo linaloendelea katika maeneo mbalimbali hapa nchni unatajwa kuwa sehemu muhimu katika kuwakinga watoto na vifo vinavyosababishwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo Donda koo, Kifaduro, Polio, Pepopunda na Surua.