Jumanne , 2nd Apr , 2019

Watu wawili wamefariki dunia na wengine  35 kujeruhiwa kufuatia ajari ya gari aina ya coster  iliyokuwa imebeba wafanyakazi wanaojenga kwenye mradi wa umeme wa Rusumo wilayani Ngara Mkoani Kagera.

Picha za tukio la ajali

Taarifa iliyotolewa na Mganga Mkuu wa wilaya ya Ngara Dr.  Revokatus Dyekobora amesema kuwa tukio hilo limetokea leo majira ya asubuhi wakati wafanyakazi hao wakielekea kazini kwao eneo la Rusumo  na  kusababisha ajari.

Amesema kuwa  hadi sasa  majeruhi  20  wamelazwa katika hospitali ya Murgwanza  na kati ya hao wawili hali zao ni mbaya na wanatarajiwa kupelekwa hospitali ya Bugando kwa matibabu zaidi, huku katika hospitali ya Nyamiaga  kukiwa na majeruhi wengine 15.

Pamoja na hayo Dk. Dyekobora ameomba watu wajitokeze kutoa damu kwa ajili ya majeruhi hao kwa kuwa damu nyingi inatuika ili kuoko maisha ya majeruhi, hivyo wasamaria wema wanaombwa kufika katika hosipitali ya Miruganzwa pamoja na ile ya Nyamiaga.

Kwa upande wake Mkuu wa jeshi la Polisi mkoani Kagera, Bw. Revocatius Malimi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba  jeshi linaendelea kufanya uchunguzi wa ajali hiyo na kwamba taarifa zaidi zitatolewa na kamanda wa polisi Mkoani Kagera .