Jumanne , 8th Dec , 2015

Halmashauri ya wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro imewasimamisha kazi watumishi tisa kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo zaidi ya shilingi milioni 515 katika kipindi cha mwezi July 2014 hadi June 2015.

Mkuu wa wilaya ya Hai akiangalia moja ya eneo la barabara ya Machame ambalo lina kasoro katika ukarabati wake huku maofisa wa Tanroads mkoa wa Kilimanjaro.

Akizungumzia kusimamishwa kwa watumishi hao kutoka idara ya uhasibu utumishi na afya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Said Mderu amesema fedha hizo zilikuwa zitumike katika ununuzi wa dawa pamoja na miradi ya maendeleo.

Bw. Mderu amesema kuwa hatua hiyo inakuja baada ya halmashauri hiyo kufanya ukaguzi wa dharura katika vitengo vya ruzuku ya miradi ya maendeleo, ununuzi wa madawa ya hospitali na mikopo ya watumishi.

Aidha mkurugenzi huyo ameongeza kuwa hatua ya kusimamishwa kazi kwa watumishi hao kutasaidia kufanyika uchunguzi huo ambao umeisabishia serikali hasara kubwa na kushindwa kuleta maendeleo kwa wakati.