Jumamosi , 21st Jun , 2014

Watu sita wamefariki Dunia na wengine 12 wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea barabara ya kuelekea Bagamoyo eneo la Makongo, jijini DSM baada ya Daladala iliyokuwa inatokea Tegeta kuelekea Mwenge kuacha njia na kugongana na daladala nyingine.

Daladala iliyopata ajali kwa kugongana na magari mengine mawili, baada ya tukio hilo.

Watu sita wamefariki Dunia na wengine 12 wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea barabara ya kuelekea Bagamoyo eneo la makongo, jijini Dar es salaam baada ya daladala iliyokuwa inatokea Tegeta kuelekea Mwenge kuacha njia na kugongana na daladala nyingine iliyokuwa ikitokea Mwenge kuelea Kunduchi.

Akiongea na East Africa Radio, Kamanda wa Mkoa wa kipolisi wa Kinondoni jijini Dar es salaam, Camilius Wambura amesema daladala hiyo inayofanya safari zake kati ya Tegeta Nyuki na Ubungo yenye namba za usajili T 441 CKT, imegongana na Daladala nyingine inayofanya safari zake kati ya Makumbusho na Kunduchi yenye namba za usajili T 377 CKT mara baada ya kukosa mwelekeo.

Kamanda Wambura amesema ajali hiyo imehusishwa magari matatu mara baada ya daladala hiyo kukosa mwelekeo ambapo miili ya watu hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Lugalo na Majeruhi wamelazwa wakiendelea na matibabu huku dereva wa daladala iliyosababisha ajali hiyo akiwa anatafutwa.