
Ugali
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Dodoma Dkt. Ibenzia Ernest amethibitisha hayo wakati akizungumza na EATV na EA Radio ambapo tayari timu imeshaenda kwa ajili ya uchunguzi.
"Ni kweli tumepokea watu 37, na tunaendelea na matibabu na walikula hicho chakula jana jioni, na walikula ugali maharage, na uzuri zaidi hakuna taarifa ya kifo." amesema Mganga wa Hospitali ya Dodoma
"Tumeshatuma wataalam ndani ya muda mfupi mtapata majibu." ameongeza Dkt. Ernest