Alhamisi , 1st Oct , 2015

Tafiti zinaonesha kuwa idadi Kubwa ya watoto chini ya miaka mitano wanakufa kutokana na magonjwa haya ya vichomi na kuhara ambayo kutokana na walezi kuchelewa kuwafikisha sehemu za tiba.

Dkt. Rukia Ally mtaalamu wa afya kutoka wizara ya afya na ustawi wa jamii.

Kutokana na hali hiyo serikali imewaagiza wataalamu wa afya kuzunguka mikoani wakianza mkoa wa Njombe ili kutoa mafunzo ya uhamasishaji kwa watoa huduma za afya ngazi ya mkoa na wilaya na kujumuisha viongozi wa serikali wakiwemo wakuu wa wilaya na wakurugenzi.

Akizungumza katika mafunzo hayo Dkt. Rukia Ally mtaalamu wa afya kutoka wizara ya afya na ustawi wa jamii amesema mafunzo hayo yatakuwa endelevu katika mikoa mingine nchini ndani ya miaka miwili.

Washiriki wa mafunzo ya mapambano ya magojwa hayo wakiwemo wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wataalamu wa afya mkoani Njombe wametoa ushauri kwa wizara kupeleka dawa mapema katika hospitali, vituo vya afya na zahanati pamoja na kubainisha gharama za mauzo ili ziwafikie walengwa mapema.

Naye katibu tawala mkoa wa Njombe Jackson Saitabau na msaidizi wake, wakati wakifungua na kufunga mafunzo hayo yaliyodumu kwa siku moja pamoja na kuwapongeza shirika linalohudumia watoto duniani la Unicef na kwa ufadhili mkubwa wanaotoa kwenye sekta ya afya amewataka washiriki kutekeleza kwa vitendo elimu walioipata pamoja na kifikisha kwa watumishi wengine wa afya na wazazi.