Jumatano , 15th Nov , 2023

Watoto watano wa familia moja Kijiji cha Nyakanazi wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera wamekufa baada ya kula chakula kinachohofiwa kuwa na sumu huku mmoja akiwa anaendelea kupatiwa matibabu hospitali teule ya Biharamulo.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Kagera Brasius Chatanda amesema kuwa watoto waliopoteza maisha ni Brian Ezekiel (3), Kahindi Samson (9), Happeness Lazaro (12), Melina Lazaro (2) na Melesiana Lazaro (11).

"Mnamo tarehe 13/11/2023 majira ya saa za usiku familia ya Lazaro Sanabanka (61) mkulima wa Kijiji cha Nyakanazi akiwa na familia yake kwa pamoja walikula chakula ambacho ni ugali mboga za majani ya maharage, baba alikula chakula akiwa na watoto watatu na watoto waliobaki walikula chakula hicho wakiwa pamoja na mama yao". Amesema Chatanda.

Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa amesema kuwa uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.

"Tumepokea kwa masikitiki makubwa sana taarifa za vifo vya watoto watano ambao wanasadikika kula chakula chenye sumu taarifa hizi zimetustua sana lakini kwa dhamana tuliyonayo kazi yetu ni kufanya uchunguzi wa kina na kuna wataalamu wanakuja kutoka nje ya mkoa kwaajili ya uchunguzi wa suala hili na " amesema Mwassa