Jumatatu , 22nd Jul , 2024

Watoto wawili wamepelekwa kwenye shule ya maadilisho mkoani Manyara baada ya kubaka na kulawiti mtoto wa miaka 6.

Watoto

Washtakiwa hao wametenda makosa mawili ya kubaka na kulawiti kwa kundi na adhabu yao ni kwa mujibu wa sheria ya watoto namba 13 kama ilivyofanyiwa mapitio 2019.

Hukumu hiyo imetolewa leo Julai 22, 2024 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya watoto iliyoko Mahakama ya wilaya ya Kiteto akiwemo Mwendesha Mashtaka Willfred Mollel

Adhabu hiyo kwa watoto hao waliolawiti na kubaka ambao ni wa miaka 15 na 16 ni kwenda shule ya maadilisho kwa miaka 3 pamoja na viboko.