Jumanne , 5th Apr , 2016

Watoto Laki Nane wanatajwa kuwa na tatizo la usonji nchini Kenya hii ikiwa ni makadirio ya Shirika linalohusika na masuala ya usonji nchini huko la Austism Society of Kenya.

Mkuu wa programu ya utafiti katika shule ya kimataifa ya Boston Higashi ilioko Boston, Marekani Dkt. John Maina,

Mkuu wa programu ya utafiti katika shule ya kimataifa ya Boston Higashi ilioko Boston, Marekani Dkt. John Maina, amesema Hata hivyo idadi hiyo inaweza kuwa juu zaidi kwa ajili ya uelewa mdogo wa tatizo la usonji na jamii nchini Kenya.

Dkt. Maina ameongeza kuwa licha ya hivyo idadi hii ni kubwa na hivyo ni lazima mikakati iwekwe ili kuwasaidia watoto hao ikiwemo na kuwapeleka shule maalumu ambazi zinawasaidia watoto wenye usonji.

Dkt. Maina amesema kuwa ni vyema watu wakafanya utafiti kuhusu watoto wao ikiwemo kuwapeleka kwa wataalamu wao ili kuweza kuwasaidi watoto na kuwajumuisha katika makundi mengine ya kijamii.

Sauti ya Mkuu wa programu ya utafiti katika shule ya kimataifa ya Boston Higashi ilioko Boston, Marekani Dkt. John Maina, akitoa ushauri wa kuwashughulikia watoto wenye usonji