
Baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi Arusha wakiwa na watoto yatima
Tukio hilo limefanyika leo Januari 28, 2023, Mkuu wa polisi wilaya ya Karatu Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Radegunda Marandu, amesema jeshi hilo limetoa misaada mbalimbali kwa yatima hao ikiwa ni mkakati wa kuifanya jamii kuwa karibu nao.
SSP Marandu amebainisha kuwa pamoja na kuwa jeshi hilo linahusika na ulinzi wa raia na mali zao pia wanalo jukumu la kushirikiana na wananchi katika matukio ya kijamii ikiwemo la kuonyesha upendo kwa yatima ambapo watakua huru kueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo za ukatili.
Sambamba na hilo pia ametoa onyo kwa watu wachache ambao wana tabia ya kuwafanyia watoto vitendo vya ukatili kuacha mara moja kwani jeshi hilo lipo makini na litachukua hatua kali za kisheria dhidi yao.
Naye Bwana Elisante Loi, meneja wa kituo hicho amesema msadaa uliotolewa utawafanya watoto hao kujua kuwa polisi ni sehemu ya jamii hivyo watakua huru kueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa jeshi hilo bila kuogopa.