Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Vodacom Tanzania Rene Meza
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Vodacom Tanzania Rene Meza amesema Tanzania ni nchi pekee ambayo wananchi wake wanalipa kodi kubwa katika sekta ya mawasiliano tofauti na nchi nyingi Afrika.
Meza amesema kwamba watanzania wanalipa kodi asilimia 38 huku nchi nyingi za Afrika zinalipa asilimia 25 hivyo kukwamisha juhudi za watanzania wengi kujikwamua kiuchumi kwani shughuli nyingi hufanyika kwa simu na Internet.
Akizungumzia huduma ya M-Pesa hapa nchini Meza amesema M-Pesa hufanya malipo yenye thamani ya shiiling Trilion 2 na hivyo kurahisisha shughuli nyingi za kiuchumi hasa maeneo ya vijijini ambapo hakuna taasisi za kifedha.
Meza ameongeza kuwa ingawa kilimo kinaajiri asilimia 74 ya watanzania wote, lakini Kilimo kinakuwa kwa asilimia 3.2 toka mwaka 2010-2013 tu na hivyo kufanya ukuaji wa uchumi usiwanufaishe wananchi wengi ambao wengi wapo maeneo ya vijijini.
Ameongeza kuwa kupitia huduma ya 'Kilimo Club' wakulima wengi kupata taarifa nyingi zinazohusu kilimo mikopo pamoja na mbegu bora.