Alhamisi , 8th Oct , 2020

Watu watano Raia wa kigeni wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam, wakikabiliwa na makosa ya kuingia nchini bila kibali.

Wa kwanza kushoto ni Askari Polisi akiongozana na washtakiwa.

Watu hao ni Adewale Oyedeji,Mnigeria,Cream Milton Elis,Mliberia,Basube Dominique,Mcongo,Ibrahim Darbey,Mliberia,Prince Tito,Mliberia, wamesomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustina Mmbando na Wakili wa Serikali Kija Elias ambapo amedai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa hilo Septemba 3,2020  katika eneo la Tegeta Jijini Dar es salaam, ambapo waliingia  nchini Tanzania bila kibali.

Katika shtaka jingine washtakiwa hao wanadaiwa Septemba 03,2020 waliingia nchini kuwa na Nyaraka zozote(VISA) huku wakijua si sahihi.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo,washtakiwa wote wamekana kutenda makosa hayo na Hakimu Mbando ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 22,mwaka huu.