Jumapili , 11th Jun , 2023

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja limefanikiwa kuwanasa waharifu watano wanaotuhumiwa kwa uhujumu uchumi baada ya kukutwa na nyaya za umeme ambazo zimeibiwa kwenye miradi ya uwekezaji na miradi ya serikali ikiwemo magaloni 20 ya mafuta ya dizeli.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja Kamishna msaidizi wa jeshi hilo ACP Daniel Shillah amesema watuhumiwa hao watano wamehusika na wizi wa nyaya hizo na wengine kushiriki kuiba magaloni ya mafuta ya dizeli, ambayo yameibiwa kwenye sehemu mbili tofauti ikiwemo kwenye ujenzi wa hotel na barabara.

Aidha Kamanda Shillah amebainisha kuwa wataendelea kuilinda miradi ya serikali kutokana na serikali kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha katika kukamilisha miradi hiyo.