Ijumaa , 2nd Oct , 2015

Viongozi wa vyama vya siasa vitano wametoa tamko la amani ambapo wamezitaka tasisi zinazojishughulisha na masuala ya utafiti kuacha mara moja kwa kile walichodai matokeo ya tafiti hizo yanawatishia wapiga kura.

Rashid Rai (katikati), akizungumza katika mkutano. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha UMD, Moshi Kigundula.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari Dar es Salaam Mwenyekiti wa chama cha UMD Taifa, Moshi Kigundula alisema asasi za kiraia ni vyema zizingatie kutunza amani ilipo badala ya kuiharibu.

Amesema ni vyema viongozi wa asasi za kiraia wakaacha kuendelea kufanya tafiti na kuwapa wagombea asilimia kishabiki bila kufuata maadili na kanuni za kitafiti.

Kwa upande wake katibu Mkuu wa Chama cha AFP, Rashidi Rai amesema viongozi wa dini zote ni vyema wakaingia katika siasa kwa ajili wa kuhamasisha amani na kutowatia hofu wananchi kwa matamko yao mbalimbali.

Viongozi hao wanatoka kwenye chama cha AFP, Chama cha UMD,Chama cha Demokrasia Makini, Chama cha CHAUSTA na chama cha Jahazi Asilia.