Ijumaa , 13th Jul , 2018

Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF) Selemani Bungara, maarufu ‘Bwege’ amefunguka kuwa anampenda mbunge wa Geita vijijini (CCM), Joseph Musukuma kwa kile alichodai kuwa ni mkweli tofauti na wabunge wengine wenye elimu kubwa.

Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF) Selemani Bungara akichangia Bungeni.

Bwege amefunguka hayo kwenye KIKAANGONI ya East Africa Television, inayorushwa kupitia ukurasa wake wa Facebook, ambapo amesema kuwa nchi ingekuwa mbali endapo wasomi wangekuwa wanazungumza kweli.

Tungekuwa mbali endapo wasomi wetu wangekuwa wanazungumza kweli, si unaona kina Lipumba sasa hivi hana hata chama , bora mimi sijasoma lakini nina Chama”, amesema Bwege.

Bwege ameendelea kuongeza kuwa, “Wabunge wa darasa la saba ninaowajua mimi ni Musukuma pamoja na Kibajaji, wale ndiyo la 7 wenzangu ambapo mara nyingi tunapiga hadithi. Nampenda Musukuma ni mkweli wakati mwingine”.

Bwege amesema kuwa mikakati ya Kilwa Kusini ni kujiinua kielimu kwa kuwa wapo nyuma sana na kupitia mazao ya Ufuta na Korosho wakulima wanachangia kwenye mfuko wa elimu.