
Rais wa kwanza wa Tanzania Julius Kambarage Nyerere, akibadilishana hati za Muungano na aliyekuwa rais wa Zanzibar Abeid Aman Karume
Wasomi na Wanataaluma nchini wameeleza hayo jana kwa nyakati tofauti ambapo wamesema mapendekezo ya serikali tatu kwa mustakabali wa taifa hayana mashiko.
Wanataaluma wa taasisi ya utafiti ya vyuo vikuu vya nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (Esaurp) Pof. Bonaventura Rutimwa, Prof Nehemiah Ossoro na Prof Ted Maliyamkono wamesema serikali moja inaweza kuwa suluhisho.
Wameendelea kudai kuwa, iwapo serikali moja itashindikana ni vyema tukaendelea kuwa na muundo wa serikali mbili ili kuwapunguzia mzigo wananchi, ikiwa ni pamoja na Zanzibar ambayo kutokana na uchumi wake haitaweza kuhimili kuchangia uendeshwaji wa serikali ya muungano.
Hata hivyo kwa baadhi ya wanasiasa, imeonekana kama njia ya Chama cha Mapinduzi kutumia Wasomi kusisitiza matakwa yao juu ya aina gani ya mfumo wa serikali ni sahihi.