Jumanne , 20th Feb , 2024

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewataka wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo na kata kufuata na kuzingatia sheria wakati wa kutelekeza majukumu yao ili uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 23 ufanyike kwa ufanisi na kupunguza au kuondoa malalamiko wakati

Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Hahakama Kuu Mhe Asina Omari

Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Hahakama Kuu Mhe Asina Omari kwa niaba ya Mwenyekiti wa Tume, wakati akifungua mafunzo kwa watendaji wa uchaguzi ngazi ya jimbo na kata zinazotarajia kufanya uchaguzi mdogo wa madiwani tarehe 20 Machi, 2024. 

Amesema uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali za kisheria ambazo hupaswa kufuatwa na kuzingatiwa kwani hatua na taratibu hizo ndio msingi wa uchaguzi kuwa mzuri na wenye ufanisi.

Asina amewaasa wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo na kata wahakikishe wanazingatia maelekezo watakayopewa na Tume badala ya kusimamia uchaguzi kwa mazoea.

"Hata kama umeshasimamia chaguzi kadhaa hapo nyuma, lakini uchaguzi huu mdogo unaojumuisha kata 23 haujawahi kuusimamia. Baada ya mafunzo hayo ndipo mtaweza usimamizi, Hivyo uzoefu wenu mkautumie kuhakikisha uchaguzi huu unafanyika kwa ufanisi wa hali ya juu," alisema Mhe. Asina.