Jumatano , 16th Sep , 2015

Watu wanne wamefariki dunia wakiwemo watatu wa familia moja na wengine 35 kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha Manga kilichopo wilaya ya Handeni mkoa wa Tanga.

Basi la Metro lililopata ajali wakati likitokea Moshi kwenda Dar es Salaam.

Tukio hilo limetokea majira ya saa tano asubuhi baada ya basi aina ya Scania mali ya kampuni ya METRO lenye namba za usajili T 244 DAF lililokuwa likitokea jijini Dar-es-salaam kwenda Rombo mkoani Kilimanjaro kuacha njia na kupinduka.

Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga ZUBERI MWOMBEJI amewataja marehemu waliopoteza maisha katika ajali hiyo na kuwaomba wakazi wa Tanga na maeneo ya jirani kujitokeza ili kuweza kuwatambua ndugu zao waliopoteza maisha katika ajali hiyo.

Justa Minja ni mmoja wa ndugu watatu wa familia moja waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo anaelezea sambamba nae Henrry Bryson ambae ni miongoni mwa wa majeruhi anaelezea namna ajali hiyo ilivyotokea