Jumatano , 26th Jul , 2023

Wanawake 200 wanaofanya biashara haramu ya kuuza miili yao wamekamatwa huku maeneo yanayotumika kwenye biashara hiyo maarufu kama madanguro 15 yakifungwa kwenye msako maalum uliofanyika katika kipindi cha miezi mitatu Wilaya ya Kinondoni.

Wamaojiuza

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya la Kinondoni Saad Mtambule , huku akihimiza kuwa msako wa kuyatafuta madanguro unaendele kwa lengo la kukomesha biashara hiyo hiyo.

"Nyumba zimesajiliwa kwa ajili ya makazi na sio biashara ya ngono, ndio maana tumewaambia waache kutumia nyumba hizo kwa matumizi hayo, lakini pia katika oparesheni tuliyoifanya tumekamata madada poa 200" Amesema DC Mtambule 

Aidha DC Saad Mtambule ameongeza kuwa jamii inatakiwa kushirikiana na serikali katika kufichua maeneo ambayo biashara hiyo hufanyika, ili mamlaka husika ziweze kuchukua hatua kali za kisheria kwa wahusika.