Alhamisi , 20th Nov , 2014

Spika wa bunge kutoka Tanzania Anne Makinda amesema wabunge wanawake nchini wamefanya kazi kubwa katika kuleta mabadiliko juu ya mtizamo wa watu kuhusu wanawake kwenye jamii.

Spika wa bunge kutoka Tanzania Anne Makinda ambaye kwa sasa ni Rais wa Bunge la Nchi za Kusini mwa Afrika, SADC.

Mh. Makinda amesema hayo jijini New York nchini Marekani katika mkutano wa Kujiandaa kwa ajili ya Bunge la SADC na kusema kuwa bunge hilo kwa sasa linajiandaa na kwa ajili kuzikabili changamoto za mabunge ya Afrika.

Spika Makinda ambaye kwa sasa ni rais wa bunge la nchi za kusini mwa Afrika SADC amefafanua wajibu wa bunge hilo Kwa kueleza kile kilichojadiliwa na kikao hicho cha maandalizi cha mkutano wa maspika kwa mwaka 2015.

Mh. Makinda amesema moja ya Agenda ambazo zitajaliwa katika vikao vya bunge hilo ni pamoja na kuona ni jinsi gani nchi zimefikia malengo ya milenia lakini pia na kuangazia masula ya Jinsia katika nchini Wanachama.