
Akiwasilisha taarifa za soko, Afisa Mauzo wa Soko hilo Bi. Mary Kinabo amesema kuwa katika kipindi hicho, idadi ya hisa zilizouzwa na nayo imepungua kwa asilimia 71 kutoka hisa milioni mbili na laki mbili hisa laki sita na sitini na tano huku kampuni ya TCC ikiongoza katika uuzwaji wa hisa zake
Bi. Kinabo ameongeza kuwa ukubwa wa mtaji wa soko umeshuka kutoka shilingi Trilioni 22 mpaka Trilioni 21 huku ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani umeshuka katika kiwango kwa asilimia mbili kutoka Trilioni 8.4 mpaka Trilioni 8.2, ambapo kiashiria cha soko kwenye sekta ya viwanda na biashara imeshuka kutoka asilimia mbili.
Afisa huyo amewataka wanafunzi wa vyuo vikuu kushiriki katika ununuzi wa hisa kwaajili ya uwekezaji kwa faida ya sasa na miaka ya baade