Mke wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Salma Kikwete.
Mama Salma Kikwete ametoa wito huo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi za kikundi cha Temeke Women Saccos (TEWE) chenye zaidi ya wanachama 100.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Temeke Mh. Abbas Mtemvu akizungumza katika uwekaji wa jiwe hilo la msingi ameishauri serikali kuvipa nguvu vikundi hivyo kwa kuwa vimekuwa vikimkomboa mwanamke wa kawaida ambaye hana uwezo wa kukopa katika taasisi kubwa za fedha.