Jumatatu , 23rd Jan , 2023

Baadhi ya wanaume na wanawake Katika Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, wamelalamikia ukatili wa kupigwa na wenza wao wa ndoa na kusababisha ndoa nyingi kuvunjia kwa kupeana talaka huku watoto wakiathirika na vitendo vya ukatili kwa kukosa malezi bora ya wazazi.

Wanaume wa mkoani Kigoma

Hayo yamebainishwa na baadhi ya Wenyeviti wa Vijiji wilayani Buhigwe, akiwemo Juma Kironda, nakuomba wiki ya sheria itumike katika kusaidia kutatua migogoro ya ndoa ambayo imeathiri ustawi wa familia na kukwamisha uzalishaji mali.

Wamesema licha ya kufanya usuluhisho, bado wanaume na wanawake wanapigwa na wenza wao wa ndoa, huku wanawake wakiomba wanaume kusimamia majukumu yao ya kifamilia.

Akizungumza wakati wa kutoa elimu ya sheria katika uzinduzi wa wiki ya sheria, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Buhigwe Katoki Venance amewasihi wananchi kutumia wiki ya sheria kutatua tofauti zilizopo na kupata haki.

Aidha Mkuu wa wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Nganyalina, amesema wilaya ya Buhigwe inakabiliwa na migogoro ya ardhi, ndoa, na mirathi na kwamba wananchi wanatakiwa kutumia uwepo wa mahakama ya wilaya kumaliza migogoro kisheria hasa kwa njia ya usuluhishi.