Jumatano , 21st Mei , 2014

Wanasiasa nchini Tanzania wametakiwa kufahamu kuwa ni jukumu lao na ni sehemu ya wajibu wao wa kila siku kuhakikisha kuwa wanawaeleza wananchi kuhusiana na athari za janga la UKIMWI nchini ili kuonesha upana wa tatizo hilo na athari zake.

Msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania, Jaji Francis Mutungi.

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania Jaji Francis Mutungi wakati alipokuwa akifunga semina ya siku mbili kuhusu maswala ya ukimwi hapa nchini iliyoandaliwa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI nchini Tanzania (TACAIDS) kwa wanasiasa hapa nchini.

Jaji Mutunga amesema ili kuwa na taifa lenye kuwa na siasa nzuri hali ya afya kwa wananchi ni lazima izingatiwe na wanasiasa wana wajibu watumie muda wao mwingi kueleza masuala yanayohusu afya kila wanapokuwa majukwaani.