Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Wanaotoa ardhi walipwe fidia - Majaliwa

Alhamisi , 26th Mei , 2022

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ihakikishe Watanzania wanaotoa ardhi yao waliyomilikishwa kihalali kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo uwekezaji wanalipwa fidia zao kwa wakati.

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa

Amesema hayo leo (Alhamisi, Mei 26, 2022) wakati akijibu swali la Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu. Mbunge huyo alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha wananchi ambao maeneo yao yamechukuliwa na wawekezaji wanalipwa fidia.

Amesema ni muhimu kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuendelea kusimamia ulipwaji wa fidia kwa wananchi waliotoa ardhi zao kwa shughuli za kimaendeleo. ”Nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kama kuna madai yametolewa na hasa kama uthamini umefanyika basi thamani ya ile ardhi iliyochukuliwa kwa ajili ya kupisha shughuli nyingine ni lazima fidia ilipwe ili haki itendeke”

Akijibu Swali ya Mbunge wa Moshi Mjini, Priscus Tarimo aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kupima maeneo ya Miji, Manispaa na Jiji, Waziri Mkuu amesema kuwa mpango huo ni endelevu wenye lengo la kupima maeneo yote nchini ili kubainisha huduma zote zinazotakiwa kutumika katika ardhi hiyo.

Majaliwa ameongeza kuwa mpango huo utakwenda hadi maeneo ya vijijini ili kuwasiaidia kupata maeneo yaliyopimwa na kutambulika rasmi ili waweze kupata hati. “Tunataka watumie hati hizi kama mtaji wa kukopea kwenye taasisi zetu za fedha, lengo ni kila Mtanzania anufaike na ardhi iliyopo, hivyo Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi iendelee kukamilisha zoezi hili, hii itawasaidia hata wawekezaji kutambua maeneo ya uwekezaji”

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali imeendelea kuhamasisha wakulima wadogo wa chikichi waendelee kulima kwa wingi zao hilo lengo likiwa ni kuhakikisha nchi inazalisha kwa wingi mafuta ya kula.

Pia, Majaliwa ametoa wito kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza kwenye kilimo hicho kwa kuwa nchi ina ardhi ya kutosha na yenye rutuba. “Ardhi tunayo, na tumeshatoa maagizo kwa wakuu wa mikoa wote kutenga ardhi kwa ajili ya uwekezaji”

“Tunataka tuzalishe na tukamue mafuta yetu sisi wenyewe, tunaamini gharama itakuwa ndogo na zile fedha tunazotumia kuagiza mafuta nje hazitakwenda tena bali tutaziingiza kwenye shughuli nyingine za kimaendeleo, uwekezaji huu ni mkubwa na endelevu”

Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Kigoma Kaskazini Assa Makanika ambaye alitaka kujua mkakati wa Serikali wa kuwakaribisha wawezaji wakubwa ili kupunguza Nakisi ya kuagiza mafuta ya kula nchini.

Majaliwa aliongeza kuwa, Serikali imeweka mkakati wa kuhakikisha inaimarisha teknolojia inayotumika katika kukamua mafuta ya chikichi “Sasa tunakwenda kuimairisha viwanda vya ukamuaji ili tuweze kukamua asilimia 99 ya mafuta kwenye chikichi badala ya 70 ya sasa”

HABARI ZAIDI

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia asema CDF mwanamke atapatikana 2030

Mratibu wa idara ya dharura (ERT) kutoka GGML, Mohamed Mwaimu akimuonesha mama lishe namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha.

Mama lishe wafundishwa kulikabili janga la moto