Jumatatu , 20th Oct , 2014

Chama  Cha Mapinduzi  kimewataka  wanachama   wake   wanaopingana  na msimamo   wa chama  hicho  kuhusu  katiba  inayopendekezwa kurudisha kadi  na kuondoka  mara  moja ndani   ya  chama  hicho.

Chama  Cha Mapinduzi  kimewataka  wanachama   wake   wanaopingana  na msimamo   wa chama  hicho  kuhusu  katiba  inayopendekezwa kurudisha kadi  na kuondoka  mara  moja ndani   ya  chama  hicho, badala  ya  kutumia mgongo  ya  CCM kuwapotosha   watanzania.
 
Kauli  hiyo  imetolewa  na  mjumbe  wa  kamati  kuu   wa  halmashauri  kuu  ya  taifa  ya Chama  Cha Mapinduzi  Mh Stephen  Wassira,  muda  mfupi  baada   ya  kupokelewa  na wawakilishi  wa wananchi  wa  mkoa  wa Mara, ikiwa ni siku  chache  tu  baada  ya  kumalizika  kwa  Bunge  Maalum  la  Katiba, ambapo amesema  kuna  baadhi  ya  wana CCM   wamekuwa  wakitumia  mgongo  wa  chama  hicho  kuwapotosha  wananchi kuhusu katiba  hiyo  inayopendekezwa.
 
Hata  hivyo  Mh. Wassira  ambaye  ni waziri  wa  nchi  ofisi  ya Rais  mahusiano na uratibu, amesema katiba  inayopendekezwa endapo   itapitishwa  na  wananchi  itajibu kilio  cha  miaka  mingi  kuhusu ukiukwaji   wa  maadili   vikiwemo  vitendo  vya  rushwa ndani  ya  jamiii.