
Mkuu wa wilaya ya Geita Wilson Shimo akiwa na wananchi katika kata ya Nyakagomba, kijiji cha Isima mkoani Geita wakati wa ziara hiyo
Mkuu wa wilaya ya Geita Wilson Shimo, amesema wapo baadhi ya watendaji wasio waaminifu ambao wamekuwa wakiwapa wazee kiwango ambacho sio sahihi na walichopokea kutoka kwenye mfuko huo.
Amewataka wazee kujifunza kusoma na kuandika ili kuepukana na changamoto hiyo huku akiagiza tume kufanya uchunguzi wa haraka kwa watendaji waliofanya dhuluma hiyo kwa kaya Zaidi ya 900 katika kata ya Nyakagomba, kijiji cha Isima mkoani humo.
Shimo ametoa maagizo hayo baada ya kupata malalamiko ya walengwa wa mpango huo katika kijiji hicho akiwa katika ziara yake ya kuhakiki fedha wanazopokea kutoka kwenye mpango huo.
Mratibu wa TASAF halmashauri ya wilaya ya Geita Gabriel Evarist amesema kutokana na changamoto ya kutokujua kusoma na kuandika ilipelekea baadhi ya wamufaika kupunjwa malipo yao ya mwezi January na February.