Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt. Samia Suluhu Hassan
"Wabunge wenu wanajua, tumejitahidi kutafuta vyanzo vya kufanya mfuko wa Bima ya Afya. Na Hasa kwenye bajeti hii waliyoipitisha hivi karibuni.
"Lakini bima ya afya ni usalama wa kila mmoja wetu. Na serikali kwa hakika, haitaweza kumsaidia kila mmoja wetu alipiwe huduma za afya," Alisema Rais Samia.
Dkt. Samia amewataka Watanzania kwa ujumla kuweka bajeti ya bima ya afya pindi watakapovuna mazao yao ili wapate uhakika wa kutibiwa mwaka mzima bure katika mahospitali yote nchini Tanzania.