Jumapili , 15th Jun , 2014

Mtandao wa jinsia nchini Tanzania TGNP umetoa tamko kuelezea kusikitishwa kwake na jinsi bajeti kuu ya serikali ilivyotenga pesa kidogo katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi.

Waziri wa fedha na uchumi Bi. Saada Mkuya Salum.

Tamko hilo limetolewa jijini Dar es Salaam leo na wanahakati wanaounda mtandao huo kutoka mikoa mbali mbali nchini, ambao wamesema licha ya serikali kutenga kiasi kisichozidi asilimia 31 ya bajeti, bado deni la taifa nalo limeendelea kukua kwa kasi ya ajabu ambapo hivi sasa limefikia shilingi trilioni 30 kutoka deni la shilingi trilioni 23 machi mwaka jana.

Kwa mujibu wa wanaharakati hao, kiasi kidogo cha bajeti kilichotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo pamoja na kasi ya ukuaji wa deni la taifa havionyeshi mweleko wa kupunguza umaskini unaowakabili idadi kubwa ya wananchi.