Jumapili , 15th Jun , 2014

Wahariri na waandishi wa habari wametakiwa kuchukua tahadhari ya kiusalama wakati wanapotekeleza majukumu yao, hasa kipindi hiki nchi inapoelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na ule wa rais na wabunge mwakani.

Mratibu wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania THRDC, Onesmo Olengurumwa.

Mratibu wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania Bw. Onesmo Olengurumwa, amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa mafunzo kwa wahariri wa vyombo mbali mbali vya habari juu ya umuhimu wa kutambua mazingira hatarishi kwa kazi zao.

Olengurumwa ametaja mazingira hayo hatari kuwa ni pamoja na kuchagua upande baina ya pande hasimu za kisiasa ambapo amewataka wahariri pamoja na wanahabari kuandika habari kwa kuzingatia miiko ya kazi yao huku wakitenda haki kwa kila upande.