Alhamisi , 5th Feb , 2015

WATOTO 380 wanafunzi walio maliza darasa la saba halmashauri ya wilaya ya Njombe hawajalipoti kidato cha kwanza licha ya kufaulu kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu kati ya wanafunzi 1310 waliofaulu.

Afisa Elimu Mkoa wa Njombe Bw, Said Nyasio

Hayo yamebainisha katika baraza la madiwani halmashauri ya Njombe na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo, Valence Kabelege wakati akifungua baraza hilo na kuwataka watendaji wa kata na vijiji kuchukua hatua.

Kabelege amesema kuwa halmashauri haijapendezwa kupokea taarifa ya watoto wengi kiasi hicho kutoenda shule, na kuagiza watendaji wa kata na vijiji kuhakikisha wanafunzi hao wanaripoti shule.

Amesema kuwa ni aibu kwa halmashauri kuwa na watoto wengi hivyo kutoenda shule watoto hao popote pale walipo watafute ili wakaanze masomo.

Amesema kuwa wanafunzi walio chaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza kwa mwaka huu ni 1310 ambapo kati yao wanawake ni 732 na wanaume 578 na wanafunzi walio ripoti shule ni watoto 862 wanawake wakiwa 466 na wanaume 396.