
Jengo la Kitivo cha Biashara Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Tamko hilo limetolewa jana Disemba 15, 2019, hii ni kutokana na kuwepo kwa sintofahamu kubwa juu ya changamoto za mikopo kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo kwani hadi sasa kuna wanafunzi hawajapata mikopo yao tangu chuo hicho kifunguliwe na kwamba yasipotekelezwa hayo yote, basi wanafunzi wenye hizo changamoto pamoja na viongozi wa DARUSO, hawatosita kuandamana hadi kwenye ofisi za Bodi hiyo.
"Wanafunzi wamevumilia vya kutosha, ahadi za uongo zimetolewa za kutosha, endapo masaa 72 yataisha bila haya kutekelezeka, wanafunzi wote wenye hayo matatizo pamoja na viongozi wa DARUSO, Disemba 19 tutaelekea kwenye Ofisi za Bodi ya Mikopo ili kudai haki zetu kwa kuwa sababu tunayo, nia tunayo na uwezo tunao" imeeleza taarifa hiyo.
Aidha taarifa hiyo imeeleza sababu za kutaka kubadilishwa kwa Afisa Mikopo wa Chuo hicho ni pamoja na kutoridhishwa na utendaji kazi wake, hasa lugha anayotumia kuzungumza na wanafunzi wanapokuwa na matatizo.