Jumatatu , 28th Nov , 2022

Watatu wakazi wa Kiteto mkoani Manyara akiwemo mwalimu wa sekondari Lesoiti, wamefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya Kiteto, kwa tuhuma za kumuua dereva bodaboda na kunyofoa baadhi ya viungo vyake kwa imani za kishirikina.

Watatu wanaotuhumiwa kumuua bodaboda

Watuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani leo Novemba 28, 2022, baada ya jitihada ya Jeshi la Polisi Kiteto kufuatilia mawasiliano yao toka awali kabla ya mauaji hayo.

Watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 21, 2022, ambapo baada ya kutekeleza mauaji yao walinyofoa viungo hivyo vya mwili wake.

Shtaka hilo limetajwa na watuhumiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uezo wa kusikiliza kesi hiyo na kesi imeahirishwa hadi Desemba 12, 2022.