Ijumaa , 13th Mei , 2022

Baadhi ya Wabunge wa Viti Maalum waliofukuzwa uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) juzi leo Ijumaa Mei 13, 2022, wameudhuria vikao vya Bunge na kuuliza maswali isipokuwa Mhe.Halima Mdee na Mhe.Ester Bulaya.

Baadhi ya wabunge hao ni Esther Matiko na Salome Makamba

Baadhi ya wabunge hao waliingia ndani ya Bunge kwa nyakati tofauti huku Mhe.Ester Matiko, akiwa wa kwanza kuingia akifuatiwa na Mhe.Salome Makamba na wengine waliingia baadaya kikao cha Bunge kuanza huku wengine wakiingia baada ya Bunge kuanza.

Leo kila mmoja ameingia na wakati wake, tofauti na mara ya kwanza walipofika kwa ajili ya kuapishwa ambapo waliingia wote 19 katika viwanja vya Bunge.