Katibu wa Chama cha Walimu Mkoa wa Arusha (CWT) Hassan Said
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Walimu hao wastaafu Mwalimu Rogathe Pallangyo na Lomayan Michael wamesema kuwa tangu wastaafu mwezi juni mwaka jana bado hawajapatiwa mafao yao ili hali mishahara yao imesitishwa jambo ambalo linazidisha hali ngumu za maisha.
Katibu wa Chama cha Walimu Mkoa wa Arusha (CWT) Hassan Said amesema kuwa kati ya walimu 31 waliostaafu katika wilaya ya Meru haifiki hata nusu ya walimu waliolipwa mafao yao hivyo wanaiomba serikali iwalipe walimu hao mafao kwa wakati ili waweze kupungu mzigo walionao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru aliyehudhuria hafla ya kuwaaga walimu waliostaafu amesema kuwa walimu wanajukumu la kuendelea kuzungumza na serikali na kukumbusha stahiki zao ili ziweze kufanyiwa kazi
Jumla ya walimu 31 wamestaafu ambapo chama cha Walimu (CWT) kimewapatia bati 20 kila mwalimu ikiwa ni mkono wa pongezi baada ya kazi ya kubwa ya kuelimisha jamii.