Jumatano , 13th Jan , 2016

Baadhi ya shule za msingi katika Manispaa ya Mtwara Mikindani zimeonyesha wasiwasi wao juu ya kasi ya wanafunzi wanaojiandikisha na darasa la kwanza kuwa kubwa na kuhofia kuzidi idadi inayokidhi mahitaji ya shule, kwa hofu ya wanafunzi kukosa kwa ku

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani, Donald Nssoko.

Wakizungumza na East Africa Radio kwa nyakati tofauti, walimu wa kuu wa shule za Kambarage na Ligula mjini humo wamesema kutokana na waraka wa elimu uliowafikia katika shule zao kuwataka wasiwakatae wanafunzi, watalazimika kuwapokea hata kama watafikia idadi inayokidhi mahitaji ya shule.

Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Mtwara Mikindani, Donald Nssoko, amesema licha ya changamoto hizo, walimu wanatakiwa kuendelea kuwapokea wanafunzi kama maagizo yanavyosema na kwamba kama kuna changamoto zozote wanatakiwa kuwasiliana na uongozi wa manispaa.

Aidha, baadhi ya wazazi walioambatana na watoto wao kwa ajili ya kwenda kuwaandikisha elimu ya msingi, wameelezea furaha yao juu ya mpango wa elimu bure na kusema umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza majukumu ya mzazi kwa mwanafunzi, huku wakikiri kuto takiwa kuchangia kitu chochote zaidi ya kutekeleza wajibu wao wa kuwaandaa watoto kwa yunifomu, daftari na kalamu.