
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. David Silinde
Naibu Waziri amesema hayo katika Kipindi cha maswali na majibu leo bungeni, nakusema kuwa Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknoloja itaajiri walimu hao.
Amesema serikali imeendelea kuajiri walimu wa Shule za Msingi na Sekondari ambapo walimu 33,684 na mafundi sanifu maabara 497 wameajiriwa kwa mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021.
Aidha Mhe. Silinde ameeleza kuwa ili kukabiliana na upungufu wa madawati katika mwaka wa fedha 2021/22 serikali imetenga bilioni 7.15 kwa ajili ya kutengeneza madawati 710,000 katika Shule za Msingi, huku ikiendelea kushirikiana na wadau pamoja na wananchi kutatua changamoto ya madawati kwenye shule za msingi na sekondari nchini.