Mtafiti Mkuu Mwandamizi wa taasisi ya wanyamapori ya TAWIRI ,Dr.Ernest Mjingo.
Tahadhari hii imekuja baada ya kuibuka kwa ugonjwa wa ebola katika nchi za Afrika Magharibi ugonjwa ambao umesababishwa na ulaji wa nyama aina ya popo ambayo imepelekea taasisi ya Nelson Mandela ya sayansi na teknolojia kuendesha utafiti ambao utainisha magonjwa ya wanyama na wanyama ambao wana magonjwa ambayo yanaweza kuhatarisha afya ya binadamu.
Akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa mradi huo wa nyamapori ,Mtafiti Mkuu Mwandamizi wa taasisi ya wanyamapori ya TAWIRI ,Dr.Ernest Mjingo amesema kuwa nyamapori nyingi hazijapimwa na zinaandiliwa katika mazingira ambayo si rafiki jambo ambalo linaweza kuhatarisha afya za walaji
Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na teknolojia cha Nelson Mandela ,Burton Mwamila amesema kuwa utafiti huo wa nyama pori utasaidia kuepusha athari zinazotokana na magonywa yanayoambukiza kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu na kusaidia kuchukua tahadhari
Kwa upande wake Mtafiti mkuu wa mradi wa nyama pori Profesa Joram Buza amesema kuwa utafiti huo utahusisha maeneo ya Serengeti,Ruaha na Seluos ambapo utafiti huo utafanyika
Utafiti wa nyama pori unatarajia kufanyika kwa kipindi cha mwaka 2015 mpaka 2017 ambapo kwa sasa utafiti huo uko katika hatua za awali na utakapokamilika utachapishwa ili kuisaidia jamii na taifa kwa ujumla ,utafiti huo utafanyika kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali ya kimataifa.