Alhamisi , 14th Jan , 2016

Wakulima wa kata ya Tungi manispaa ya Morogoro wamesema watalima kwa nguvu kwenye shamba la mwekezaji wa Tungi Estate inayoshugulika na kilimo cha katani.

Wakulima wa kata ya Tungi manispaa ya Morogoro wamesema watalima kwa nguvu kwenye shamba la mwekezaji wa Tungi Estate inayoshugulika na kilimo cha katani kufuatia uongozi wa wilaya kushindwa kuwatetea dhidi ya mwekezaji huyo.

Wakulima hao wanadai kuwa mwekezaji huyo anawanyima mashamba ya kulima na kusababisha kuishi kwa tabu ikiwa ni pamoja na kukabiliwa na baa la njaa.

Wakizungumza kwa jazba wakiwa shambani humo wakulima hao wamesema kuwa wamechoshwa na serikali ya halmashauri ya manispaa, wilaya na mkoa kuendelea kuwakumbatia wawekezaji huku wananchi wakiteseka kwa kukosa maeneo ya kulima.

Wamesekwamba eneokubwa limehodhiwa na mwekezaji wa shamba la katani hivyo wameiomba wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi kuingilia kati mgogoro huo.

Diwani wa kata ya tungi bwana juma tembo amewataka wakulima hao kuwa watulivu wakati wakishugulikia tatizo hilo huku mkuu wa wilaya ya Morogoro bwana Muhingo Rweyemamu akikiri kuwepo mgogoro huo ingawa amesema wakulima hao walimuomba amuandikie mwekezaji barua ya kumuomba awaruhusu kulima katika shamba hilo.

amewataka wananchi hao kuacha mara moja tabia ya kuvamia mashamba ya watu kwa kisingizio cha kutaka kulima na watakao thubutu kufanya hivyo watachukuliwa hatua kali