Alhamisi , 23rd Jun , 2016

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba, ameiagiza bodi ya Soko la Mahindi la Kimataifa la Kibaigwa, na Uongozi wa Halmshauri ya Kongwa kuweka utaratibu utakaowawezesha wakulima kuuza mazao yao bila kudhurumiwa kutoka kwa madalali.

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba,

Waziri Dkt. Tizeba ametoa agizo hilo mara baada ya kutembelea soko hilo na kuzugumza na viongozi Wakulima, wafanyabiashara na madalali katika soko la Kimataifa lililoko katika wilaya ya Kongwa, Mkoani Dodoma.

Dkt. Tizeba amesema kuwa mfumo uliopo sasa unauwezekano mkubwa wa kutokea udanganyifu kwa wakulima kutoka kwa madalali kwa kuwa mahindi yao yameuzwa kwa bei ya chini tofauti wakati inawezekana jambo hilo si la kweli.

Aidha ameitaka bodi hiyo kudhibiti msururu wa Ushuru unaowazonga wafanyabiashara hao wa mahindi ikiwa ni pamoja na kulipa ushuru sehemu moja tu ili kulinda kilimo cha zao hilo ili kuleta tija kwa wafanyabishara hao.

Kwa upande wako wakulima na wafanyabiashara wa Mahindi wamesema kuwa uwepo wa mtu wa kati katiba biashara hiyo ya mahindi ina chagamoto kubwa ya uaminifu katika bei halisi ya mahindi kwa wateja wanaowauzia mbali na eneo la soko hilo.

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba,