Mbunge Zungu ameyasema hayo Bungeni mjini Dodoma wakati akichangia mpango wa serikali kwa mwaka 2016 & 2017, kikao cha 7 cha bunge la 11 linaloendelea na vikao vyake kwa mujibu wa sheria.
''Mheshimiwa mwenyekiti nataka mawaziri husika wanisikilize na waelewe kwamba taarifa ambazo wanapewa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kuhusu wananchi kupewa viwanja mabwepande si za kweli'' Amesema Zungu.
Mbunge huyo ameongeza kuwa hakuna wananchi waliokimbia au kukataa au kuuza viwanja kama taarifa za ofisi ya mkuu wa mkoa inavyosema na kupewa mawaziri, hivyo suala hili tulitizame upya.
Katika kuchangia suala hilo hilo pia leo mbunge wa Kawe Halima Mdee CHADEMA ameitaka serikali iangalie utaratibu wa mkaguzi mkuu wa serikali kufanya ukaguzi wa viwanja vilivyotolewa kwa wananchi wa mabondeni waliopewa viwanja baada ya kukumbwa na mafuriko miaka 4 iliyopita maana hakuna uhalisia wa wananchi na viwanja vilivyotolewa.



