
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani
Akizungumza leo katika uzinduzi wa kiwanda Multi Cable Limited (MCL) kinachozalisha mita za Luku za umeme Dkt. Kalemani amesema upungufu wa mita hizo ndio ulikuwa unachelewesha usambazaji umeme ambapo kwa sasa zipo za kutosha hivyo hakuna kisingizio cha ucheleweshaji wa usambazaji wa huduma hiyo.
"Wako watanzania takribani 5,100 wamelipia umeme na bado hawajaunganishiwa wakati sababu mita za umeme hazipo naomba nielekeze kwa mkurugenzi Mkuu wa TANESCO na REA pamoja na mameneja wote wa kanda ,mikoa na wilaya wawaunganishe wateja wote waliolipia ndani ya siku 21 kuanzia leo atakayeshindwa kuunganisha jambo la kwanza ujiuzulu kwa hiari yako", amesema Dkt Kalemani.
Dkt. Medard Kalemani amesema kuwa serikali itahakikisha inasimama bega kwa bega na wazalishaji wa viwanda vya kutengeneza Luku ikiwemo kwenye suala kuwatafutia masoko ili kulinda bidhaa zinazotengenezwa nchini na kukuza solo la ndani.
Aidha, Waziri huyo amewataka wazalishaji wa mita za umeme chini kuanzisha kuzalisha mita za phase tatu ili kuwasaidia wenye viwanda vidogo huku akitoa marufuku kwa vifaa vinavyotengenezwa nchini kusambazwa nje nchi.
Uzinduzi wa kiwanda hiki unakamilisha jumla ya Viwanda 10 vilivyopo nchini ambavyo vinatengeneza mita za luku ya umeme.