Jumatano , 20th Jul , 2016

Wajasiriamali Wanawake wa Dar es Salaam wamesema kuwa kukosekana kwa maeneo rasmi ya kufanyia biashara zao ni tatizo katika kukuza na kuendeleza shughuli zao.

Mmoja wa wajasiriamali akionyesha bidhaa zake.

Akiongea jana Jijini Dar es Salaam kwa niaba ya wajasirimali wanawake 510 waliohitimu mafunzo ya Mpango wa kukuza ujasiriamali na biashara kwa Wanawake(MKUBWA), Bi. Halima Kinabo, amesema wanakabiliano na changamoto nyingi katika kuendesha biashara yao.

Bi. Kinabo amesema kuwa tatizo jingine ni upatikanaji wa vitendea kazi ikiwemo mashine za kuzalishia bidhaa ndogo ndogo pamoja na kukosa mitaji ya kutosha kuendeleza biashara zao.

Aidha ameongeza kuwa Pia taasisi zinazotoa mikopo zinatoza riba kubwa ambazo ni vikwazo kwa wajasirimali wadogo kupata mikopo hiyo huku pia upatikanaji wa vifungashio bora kuwa kikwazo kwa biashara kuonekana hazina ubora.